#HABARI: Elimu ya msaada wa kisheria inayotolewa kwa wananchi kupitia Kampeni ya Mama Samia Legal Aid imeanza kuzaa matunda mkoani Shinyanga huku wananchi wakikumbushwa kujenga tabia ya kuandika wosia.
Hali hiyo imebainishwa katika Kijiji cha Mahembe Kata ya Mwakitolyo Wilayani Shinyanga, baada ya wataalamu wa Sheria kutoka katika kampeni ya Mama Samia Legal Aid kufika katika kijiji hicho na kutoa elimu ya sheria.
Aidha, wananchi hao wamesema jamii yao iilikuwa inakabiliwa na migogoro mingi ikiwemo migogoro ya ardhi, Mirathi na ukatili wakijinsia hali ambayo baada ya elimu ya Mama Samia legal Aid, imeanza kuonekana kupungua.
Wakitoa elimu ya msaada wakisheria kwa wananchi hao, baadhi ya wanasheria hao, wamewataka wananchi kujenga tabia ya kuandika wosia ili kuepusha migogoro ya ndugu kuwania mali watakazoziacha endapo ikitokea wamefariki dunia.
Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Mwakitilyo Insp. Gerald Nyankanga, amesema elimu hiyo imesaidia kupunguza matukio ya uvunjifu wa amani yanayofikishwa kituoni hapo akiwaeleza wananchi hao watumie elimu hiyo kuboresha mahusiano yao katika jamii.
(Feed generated with FetchRSS)
