#MICHEZO: Lamine Yamal ametajwa kuwa Mchezaji Bora Chipukizi Duniani katika hafla ya Laureus World Sports Awards 2026 iliyofanyika katika Palacio de Cibeles, Madrid.

Katika hafla hiyo iliyoongozwa na Novak Djokovic na Eileen Gu, Yamal (18) aliweka historia kwa kuwa mshindi mdogo zaidi kushinda tuzo hiyo mara zaidi ya moja tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.

Nyota huyo wa FC Barcelona amekuwa na msimu bora, akifunga mabao 23 na kutoa pasi za mabao 17, huku akiisaidia timu yake kutwaa mataji ya La Liga, Copa del Rey na Supercopa de EspaƱa.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *