#MICHEZO: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, ameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni 50 kwa timu ya mpira wa kikapu ya Dar City Basketball endapo itafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwenye mashindano yanayotarajia kutimua vumbi jijini Kigali, Rwanda.
RC Chalamila ametoa motisha hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal 3, wakati akiwasindikiza na kuwaaga wachezaji wa timu hiyo kuelekea kwenye mashindano hayo.
Katika hafla hiyo, Mhe. Chalamila ametoa rai kwa wakazi wa Dar es Salaam kuwapeleka ofisini kwake vijana wote wenye vipaji vya mpira wa kikapu ili waendelezwe na kuunganishwa na nguli wa Dar City.
Aliongeza kuwa, mara baada ya Rais wa timu hiyo, Ndg. Hashim Thabit, kurejea kutoka Rwanda, utaratibu utafanywa ili akutane na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wa mkoa huo kwa lengo la kuweka mikakati ya kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa wa mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, ameipongeza Dar City akitaja kuwa ni timu ya kihistoria na ya kimataifa tangu nchi ipate uhuru, huku akiwatakia kila la heri katika kuipeperusha vyema bendera ya Taifa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)
