Meneja Msaidizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja AzamPesa, Jacqueline Magesse ameeleza kuwa maboresho ambayo yamefanyika kwenye huduma ya AzamPesa ni pamoja kumpa mteja uwezo wa kutuma pesa kwenda mitandao yote na benki bure bila makato yoyote.
Magesse amezungumza hayo leo kupitia kipindi cha #MorningTrumpet, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja, ambapo amezungumzia mambo mbalimbali katika mahojiano hayo yanayopatikana kwenye ukurasa wetu wa YouTube wa #UTVTanzania.
✍Nifa Omary
Mhariri | @abuuyusuftz
#AzamTVUpdates #MorningTrumpet #utv108