Tangu Aprili 2023, mvutano wa madaraka kati ya Mkuu wa Jeshi, Abdel Fattah al-Burhan na aliyekuwa naibu wake Mohamed Hamdan Daglo, ambaye ni kiongozi wa kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF), umegeuka kuwa moja ya migogoro mikubwa ya kibinadamu duniani, kama inavyoelezwa na Umoja wa Mataifa.
Kuanguka kwa mji wa El-Fasher tarehe 26 Oktoba, baada ya wapiganaji wa RSF kuuteka mji huo ambao ulikuwa kituo kikubwa cha mwisho cha Darfur Magharibi kisichokuwa chini ya udhibiti wao, kuliashiria hatua muhimu katika vita ambavyo tayari vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu, kuwahamisha karibu watu milioni 12 na kuibua mgogoro mkubwa zaidi wa uhamishaji na njaa duniani.
#AzamTVUpdates
✍Jairo Mtitu
John Mbalamwezi