Rais Samia awazawadia Tanzanite Queens Sh50 milioniRais Samia awazawadia Tanzanite Queens Sh50 milioni

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda amesema kuwa Rais Samia amefurahishwa na mafanikio hayo na ameona awashike mkono wachezaji na benchi la ufundi la Tanzanite Queens.

“Niwapongeze U20 (Tanzanite Queens) kwa kufuzu Kombe la Dunia. Tumepokea maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo Wizara tunayafanyia kazi.

Pamoja na kwamba BMT na TFF katika kuzisimamia timu za taifa. Rais amewiwa kuwapa motisha U20 ambao wamefuzu Kombe la Dunia kiasi cha Sh50 milioni ikiwa ni sehemu ya motisha kwa kazi waliyofanya ya kuipa heshima Tanzania kimataifa.

“Kwa niaba ya Rais tunawapongeza na mjue kwamba bado anaendelea kubeba gharama za timu za taifa akishirikiana na TFF pamoja na BMT,” amesema Makonda.

Makonda ameyasema hayo katika hafla ya chakula cha mchana aliyomuandalia nyota wa zamani wa Manchester United na England, Rio Ferdinand, leo Jumatano, Mei 20, 2026 jijini Dodoma.

Ferdinand azipongeza Tanzanite Queens, Serengeti Boys

Ferdinand ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku tatu, ameshukuru mapokezi aliyopata nchini na amezipongeza Tanzanite Queens na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kwa kufuzu Kombe la Dunia.

“Asante sana kwa mapokezi niliyopata tangu nilipowasili. Ninashukuru sana kwa jinsi nilivyokirimiwa.

Nawapongeza timu ya wanawake kwa kufuzu Kombe la Dunia. Ni mafanikio makubwa. Nitakuwa tayari kuleta mabadiliko chanya,” amesema Ferdinand.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *