Dodoma.
Hospitali ya Serikali ya Benjamini Mkapa (BMH) Jijini Dodoma imeanza huduma ya upandikizaji uume kwa wanaume wenye matatizo ya uume kutofanya kazi sawa sawa.

Kwa mujibu wa hospitali hiyo, huduma hiyo inahusisha uume usiosimama sawa sawa kwa kuuwekea kifaa maalum kinachofanana na ‘jeki’ ili waendelee kufurahia tendo la ndoa kama kawaida.

Akizungumza na wahariri wa vyomb vya habari waliotembelea hospitalini hapo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt Abdalla Baja amesema huduma hiyo imeanza kutolewa mwaka 2023.

“Mpaka sasa tumeshawafanyia upandikizwaji wa uume wagonjwa 13 na wanaendelea kuheshimisha ndoa zao hapa Tanzania,” ameongeza Dkt Baja.

Akizungumzia gharama Dkt Baja amesema ili mgonjwa apandikizwe uume itamgharimu kiasi cha Sh10 milioni.

“Unajua tatizo la kutosimamisha uume sawa sawa wanapata watu wengi ila shida ni unyanyapaa, mgonjwa anaanza kujinyanyapaa mwenyewe hawezi kuja hospitali kupata matababu. Niwatie moyo wanaume wenzangu wale ambao jogoo halipandi mlima sawasaa msiogope sasa mkombozi amepatikana. Benjamini Mkapa hospitali tumeliona hilo na na wahakikishia heshima ya ndoa zenu zitarudi kama zamani,” amesisitiza Dkt Baja.

*Meandaliwa na Caren Tausi Mbowe*

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *