BENKI ya CRDB kupitia kampuni yake tanzu ya CRDB Bank Foundation, imezindua rasmi msimu wa saba wa CRDB Bank International Marathon 2026, utakaofanyika Agosti 2026 jijini Dar es Salaam na kupambwa na uzinduzi wa tamasha jipya la kimataifa la burudani lijulikanalo kama IMBEJU Sauti Moja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela, amesema mafanikio ya CRDB Bank Marathon yamedhihirisha kuwa ukuaji wa biashara unakuwa na maana zaidi unapokwenda sambamba na uwekezaji katika ustawi wa jamii.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema Tamasha la IMBEJU SAUTI MOJA itanogesha CRDB Bank Marathon 2026 ambapo pia Washiriki wote wataruhusiwa kufanya vipimo vya moyo bure katika kituo chochote cha JKCI.

Katika hatua nyingine Kampuni za Utangazaji za Star Tv, Radio Free Africa na Kiss FM zimekuwa miongoni mwa washirika muhimu wa mbio hizo.

Kupitia marathon hiyo, mamia ya watoto wenye changamoto za moyo na wakina mama wenye ujauzito hatarishi wamepata huduma za matibabu, huku maelfu ya vijana wakinufaika na mafunzo, uwezeshaji na fursa za kiuchumi kupitia IMBEJU.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *