Uganda yawaweka karantini zaidi ya watu 100 huku WHO ikitoa tahadhari kuhusu kasi ya Ebola
Serikali ya Uganda inasema zaidi ya watu 100 wamewekwa karantini huku maafisa wa afya wakijitahidi kudhibiti mlipuko nadra wa Ebola unaohusishwa na aina ya virusi vya Bundibugyo.